Rais Samia alisisitiza kuwa matukio ya maandamano hayo-ngawa yalikuwa na athari za muda mfupi-hayakubadili misingi ya umoja wa nchi, bali yalitoa nafasi ya kujifunza, kuimarisha mifumo ya mawasiliano, ushirikishwaji wa wananchi, na kuendelea kujenga demokrasia yenye uwiano na utulivu.

2 Desemba 2025 - 17:37

Rais Samia Awaongoza Wazee wa Dar es Salaam Kujadili Mustakabali wa Taifa Baada ya Uchaguzi 2025 +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, ameshiriki katika Mkutano Maalum wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika leo, Jumanne, Desemba 2, 2023, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umehudhuriwa na wazee kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam, viongozi wa chama na Serikali, pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya kijamii na kisiasa. Lengo kuu la mkutano lilikuwa ni kutoa fursa kwa wazee-ambao ni hazina ya busara, uzoefu na uadilifu-kuzungumza, kushauri na kuchangia maoni kuhusu mwenendo wa nchi na mustakabali wa Taifa.

Hotuba ya Mgeni Rasmi: Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alitumia nafasi hiyo kuzungumza na wazee kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa, hususan yale yanayohusu:

  • Hali ya siasa nchini baada ya Matukio ya Maandamano yaliyofuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025;
  • Changamoto zilizojitokeza katika kipindi hicho na namna zilivyoweza kudhibitiwa;
  • Hatua za Serikali katika kuhakikisha utulivu, ustawi wa kisiasa, na kudumisha taswira ya Tanzania duniani kama nchi ya amani, umoja na upendo.

Rais Samia alisisitiza kuwa matukio ya maandamano hayo-ngawa yalikuwa na athari za muda mfupi-hayakubadili misingi ya umoja wa nchi, bali yalitoa nafasi ya kujifunza, kuimarisha mifumo ya mawasiliano, ushirikishwaji wa wananchi, na kuendelea kujenga demokrasia yenye uwiano na utulivu.

Umuhimu wa Wazee Katika Mwelekeo wa Taifa

Katika mkutano huo, Rais Samia pia aliwatambua wazee kama nguzo muhimu ya Taifa, akisema kuwa:

  • Wazee wana mchango mkubwa katika maadili ya kitaifa,
  • Ni washauri wakuu katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa,
  • Na wana uwezo wa kuongoza vijana kuelekea katika misingi ya uzalendo, uadilifu na mshikamano.

Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ya ushiriki wa wazee katika mchakato wa maamuzi, ili kuimarisha umoja na maendeleo ya Taifa.

Rais Samia Awaongoza Wazee wa Dar es Salaam Kujadili Mustakabali wa Taifa Baada ya Uchaguzi 2025 +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha